Kwa ambaye bado hana taarifa, BRELA sasa hivi haipokei tena nyaraka ngumu (hard copies) zozote. Kila kitu sasa kinafanyika kwenye mtandao kwa kupitia mfumo unaoitwa Online Registration System (ORS).

Kampuni zote ambazo zilikuwepo kabla ya mfumo huu mpya kuanza zinatakiwa kujisali kwenye ORS. Kampuni isipofanya usajili huo haitaweza kupatiwa huduma karibu zote muhimu kutoka BRELA. Haitaweza kuwasilisha annual returns wala nyaraka nyingine, mabadiliko yoyote itakayoyafanya hayatapokelewa BRELA na itakuwa vigumu kufanya mambo mengine mengi.

Vilevile, kampuni inaposhindwa kuwasilisha annual returns au nyaraka nyingine ndani ya muda unaotakiwa, itawajibika kulipa faini kwa kila mwezi uliochelewa. Miezi ya kuchelewa inavyozidi kusogea, faini nayo huongezeka hadi kufikia kiwango kikubwa sana.

Hivyo basi, ili kuepuka usumbufu wote huo, ni muhimu sana kampuni husika kufanya usajili mapema.

Katika kufanikisha usajili huo, ukiacha taarifa binafsi za shareholders, directors na company secretary, mahitaji mengine muhimu kwa ajili ya usajili kwenye ORS ni:-

  • Kitambulisho cha NIDA (kwa Watanzania). Company secretary, kila shareholder na kila director anatakiwa awe na hicho kitambulisho, la sivyo usajili hautakamilika. Kama hauna ID ya NIDA, kuna kibali maalum kutoka BRELA cha kukuwezesha kupatiwa hiyo ID mapema.

Raia wa kigeni wanatumia passport zao.

  • TIN iliyohakikiwa (kwa watanzania). Company Secretary, kila shareholder na kila director anatakiwa awe na ID ya NIDA, na pia awe na TIN iliyohakikiwa.

Raia wa kigeni wanatumia passport zao.

  • Nakala ya annual returns ya mwaka uliopita.
  • Nakala ya audited accounts za mwaka uliopita.

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia info@matrix.co.tz